Habari...
Software Support Tanzania inapenda kutoa masomo mbalimbali yanayohusiana na teknolojia za simu na computer na leo tunapenda kujulisha wafuatiliaji wetu kuhusu jinsi ya kufufua au kuzirekebisha Memory card, USB flash, External storage, zote zilizokufa na kushindwa kutumika tena.
MUHIMU
- Kuwa makini kwenye kila hatua.
- Utakapo kosea kuandika drive letter ya flash yako itapekea kufuta vitu visivyo husika kwenye partion zako.
- Software Support Tanzania hatutohusika kwa uzembe wowote ule na uharibifu wowote.
MAHITAJI.
- Kompyuta
- USB iliyokufa.
NJIA YA KWANZA
Kama tulivyosema unahitajika umakini katika kila hatua.HATUA
- Chomeka USB Flash yako iliyokufa kwenye computer.
- Nenda kwenye My Computer, Angalia jina la Flash (drive letter) Mfano drive letter J:
- Bonyeza Window + R Kisha andika CMD na ubonyeze Enter
- Andika J: kisha bonyeza Enter(J: ni drive letter ya flash yako)
- Andika J: format kisha bonyeza Enter
- Itakuuliza chagua kati ya (Y/N) bonyeza Y kukubali ikimaanisha Yes
- Subiria imalize mpaka 100%, itakuletea ujumbe format completed.
- Andika neno exit kisha bonyeza enter, ilikuondoka kwenye CMD.
Njia hii mara nyingi utatua sana matatizo ya memory card kuliko vifaa vingine vyote pia huondoa write protection kwenye memory card.
NJIA YA PILI
HATUA- Chomeka USB Flash iliyokufa kwenye computer.
- Nenda kwenye My Computer, Angalia ukubwa ( Size ) ya Flash Mfano Removable disk J: (7.5GB)
- Bonyeza Window + R Kisha andika CMD na bonyeza Enter
- Andika diskpart kisha bonyeza Enter
- Andika List disk kisha bofya Enter
Kama inavyoonekana hapo chini

Mara nyingi disk 0 huwa ni Hard disk yako total storage hivyo uwe makini usiichague hiyo
7. Angalia namba ya kifaa unachohitaji kukifufua kisha Andika Select disk namba
ya kifa kama kilivyosoma.
Mfano Kma flash yako imeoneshwa disk 1 au disk 2 itakuwa hivi
select disk 1 au select disk 2 kisha bonyeza Enter
8. Andika Clean kisha bonyeza Enter
9. Andika create partition primary kisha bonyeza Enter
10.Andika active kisha bonyeza Enter
11. Andika select partition 1 kisha bonyeza Enter
12. Andika format fs=fat32 kisha bonyeza Ente.
13. Bonyeza link hapa chini kuangalia hatua ya mwisho
Mpaka hapo utakuwa umefanikisha kukufua kifaa chako kilichokuwa kimekufa na kuanza kukukitumia tena kwa mara nyingine
Njia zote mbili hapo juu zinafanya kazi vizuri kama Kifaa chako hakitokuwa write protect
Download App Yetu hapa Chini
USISAHAU KUSHARE MAKALA HII NA WENZIO.
Imeandaliwa na SOFTWARE SUPPORT TANZANIA
Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana nasi kupitia
Facebook Page: Software support Tanzania
Instagram: Softwaresupporttanzania
Email: softwarestanzania@gmail.com
BLOG: http://softwaresupporttz.blogspot.com/
Don’t forget to subscribe our BLOG and Youtube channel Software support Tanzania
Usisahau ku-share kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Asante kwa kutumia huduma zetu
Software Support Tanzania

