Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Test link

JINSI YA KU-UPDATE ANDROID VERSION KUTOKA KITKAT MPAKA LOLLIPOP





Habari...

Software Support Tanzania Leo Inapenda kuwajuza ni Jinsi Gani unaweza Ku-update Au Kuongeza ububwa wa Android Version Ya Simu yako kwa kutumia ROM Husika kulingana na Kampuni Husika Simu.
.
MAHITAJI
  • Orginal Memory Card (8GB)
  • Bandle la MB (1GB)
  • Simu Husika Iwe Rooted
MUHIMU
  • Zoezi ili ni la hatari ukikosea unaweza kuuwa Simu Yako
  • Software Support Tanzania Hatutohusika kwa uharibifu/uzembe wowote utakaojitokeza
  •  Hakikisha simu ina Chaji ya kutosha. Inashauriwa wakati waku-update iwe kwenye chaji. 
  • Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu yako.  Nenda Settings =>About phone =>Build number
    AU
    Nenda Settings=>About phone =>Software information =>Build number. Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba (tap 7 times)…mpaka upate ujumbe huu “You are now a Developer” Sasa nenda Settings>Developer options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama haipo). Hatua hii kwa wengi hua ni tayari kwani hufanywa wakati wa ku root.

Kwa Kawaida Simu Zote za Smart Phone utengenezwa na kutofautishwa kwa mifumo mikuu mitatu ifuafatayo(Operating system).

Amabyo ni:
  • Mfumo wa Android
  • Mfumo wa iOS
  • Mfumo wa Window Phone
Kuna Ushindani Mkubwa sana kati ya mifumo hiyo na kila mmoja umzidi mwenzie kulingana na mahitaji ya watu/ubora/urahisishaji/matumizi n.k hali hii usababisha uboreshaji wa vitu kwa kila mfumo.
Simu Zenye mfumo wa Android ndizo simu pekee zinazotumika na idadi kubwa ya watu Duniani kote kwa sababu tofauti toauti.

Baadhi Ya Sababu Zinazo Sababisha Mfumo Wa Android Kutumiwa na idadi ya Watu wengi Duniani 
  • Kuna Application Nyingi na za Kisasa Zenye Kazi Tofauti tofauti amabazo bado watumiaji wa iOS hazijawafikia.
  • Ni rahisi sana Ku-Root Simu za Android na kuzitumia Utakavyo.
ROOTING ni kitendo cha kukupa uwezo wa kutumia na kuifurahia simu yako kwa asilimia mia moja. Ukisha root simu yako unakua na uwezo wa ku UPDATE mfumo wa simu yako Mfano kutoka Kitkat kwenda Lollipop, kuweka Application Zilizozuiwa na Android Developers 

Mfano
Application  maalum za Kutunza Chaji, ku-boost simu yako, kukuongezea RAM, Application  za kukuwezesha kuipata simu yako hata pale mwizi anapoi flash), kutoa ‘System applications’ ambazo huna kazi nazo, kuufanya mfumo wa simu UWE KAMA UTAKAVYO wewe n.k
  • Simu zinazotumia mfumo huu zinauzwa kwa Grarama ndogo zikilinganishwa na zinazotumia iOS na Windows phone.
  • Kuna zaidi ya Program 1.6 million zinazofanya kazi kwenye mfumo huu amabazo mtumiaji anaweza kuzitumia kwenye simu yake kuendana na Mahitaji yake.


Kwa waliobahatika kuisoma makala yetu JINSI YA KU ROOT SIMU YAKO YA ANDROID, nafikiri tunaelewana  zaidi hapa.

Mfumo Wa Android una Matoleo yafuatayo hadi Makala hii inapoandikwa ambayo ni:
  • Cupcake (1.5)
  • Donut (1.6)
  • Éclair (2.0 – 2.1)
  • Froyo (2.2 – 2.2.3)Gingerread (2.3 – 2.3.7)
  • Honeycomb (3.0 – 3.2.6)
  • Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)
  • Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)
  • KitKat (4.4 – 4.4.4)
  • Lollipop (5.0 – 5.1.1)
  • Marshmallow (6.0 --- )
  • Nougat (7.0-7.)
KUJUA TOLEO LA SIMU YAKO

Nenda SettingsAbout phoneAndroid version.

Software Support Tanzania Tunatoa na kufundisha makala hii Kwa sababu zifuatazo

UMUHIMU WA KUWEKA MFUMO WA LOLLIPOP
  • Mfumo wa Lollipop ni ‘stable’ na fasta kuliko KitKat
  • Unatunza chaji kuliko Kitkat kwani ‘bugs’ nyingi zimekua fixed na pia ‘Power saving feature’ imeboreshwa
  • Una mwanga zaidi (More brighter) na pia una Visual effects nzuri na za kuvutia
  • Una uwezo wa ku manage app nyingi bila ujumbe wa ‘program not responding’ au ‘Unfortunately, program has stopped’
ili kufanikisha zoezi ili Fuata Hatua Zifuatazo

HATUA

1. Root Simu Yako

2. Nenda settings=> Security=> Unknown Sources. Weka tiki hapo (Kama haipo).

3. Nenda Playstore install program inayoitwa [ROOT] Rashr – Flash Tool. Usiifungue baada ya kui Install.

4. Hatua hii ni ya Muhimu sana. Kabla hatujaiangalia tunapaswa kujua vitu vinne vya Muhimu.

  • Recovery: Hiki ni kipengele cha Mfumo wa simu au hata Computer ambacho kimetenganishwa na Mfumo wa kawaida wa simu. Hiki husaidia tunapo flash/ku update simu.
  •  Bootloader ni sehemu ya Mfumo wa simu na hata Computer ambacho ndicho huamua Simu au Computer kuwakia kwenye Recovery  Mode au iwake kawaida. Kwa wale wanao Install Windows OS kwenye Computer zao wanatuelewa  zaidi hapa. Unapoweka DVD ya Windows files na kuwasha PC yako na Kubonyeza F12 Key. Hapo ni kwamba unai Instruct PC yako iwake kwenda kwenye Recovery. Ndicho tunachokifanya tunapo Install Android Lollipop ROM.
  •  ROM (Operating System Image) : ni Flash files ambazo ndizo huwekwa kwenya Read Only Memory (ROM) ili simu iweze kuwaka.
  • Android Custom Recovery. Watengenezaji wa Simu za Android wame lock Bootloader ili watumiaji wake wasiweze ku Install ROMs mbalimbali kwenye simu hizo. Wameweka Recovery ambayo hairuhusu kuflash chochote.
5. Ku Unlock Bootloader ili tuweze ku flash ROM yoyote kwenye simu ya Android.
Kufanikisha hatua hii tuna flash Android Custom Recovery nyingine itakayoturuhusu kuflashia ROM mpya Kwenda kwenya Mfumo wa simu. Zipo Android Custom Recovery mbili (2) ambazo hutumika sana tunapo flash Android Devices ambazo ni
  1. ClockworkMod Recovery (CWM) 
  2. Team Win Recovery Project (TWRP)
Software Support Tanzania  tunanashauri utumieTWRP kwani ni rahisi kutumia, inaeleweka zaidi pia ina Option nyingi.

HATUA ZA KU-INSTALL TWRP

  1. Kwa kutumia simu yako au PC, nenda google kisha search tmrp ya Simu yako. Mfano kama unatumia Tecno H6, search ‘twrp image for Tecno H6’ au ‘Team Work Recovery Project image for Tecno H6’ kisha i download.
  2. Ukishai download iweke kwenye Memory Card ya simu unayotaka kuiflash
  3.  Fungua Rashr (rejea hatua ya nne hapo juu) kisha gusa ‘Recovery from Storage’. Hapo chagua twrp ulioi download na kuiweka kwenye memory card. Kisha Gusa ‘Yes’ utakachoulizwa. Kama itakua imefanikiwa Utaona ‘ Partition flashed. Reboot into Recovery now?’ Gusa ‘NO’ Kisha nenda hatua ya 6.

6. Download  Lollipop ROM kwa ajili ya SIMU YAKO. Ziko ROMs nyingi kutoka kwa Developers tofauti.
Binafsi tulishakutana nazo nyingi na asilimia kubwa zilikubali lakini nyingine hua zinakataa!! Nenda Google kisha search ROM ya Simu yako…Mfano kama unatumia Tecno H6; search ‘Lollipop ROM for Tecno H6’ Nyingi hua ni zaidi ya MB 300.

TAHADHARI;

Kabla ya ku download ROM utakayoiona tunashauri usome kwanza Maoni ya  walioitumia ili uweze kujua kama ilikubali kwao. Baadhi ya ROMs hua zilishakua infected na Virus na ukizi Install hua zinakataa!! Na zikikataa hua nia HATARI kubwa kwani simu haitawaka tena! Baada ya kui download iweke kwenye Memory Card ya Simu unayotaka kui flash/update.

7. Fungua tena Rashr kisha gusa ‘Reboot Recovery’. Sasa simu yako itawakia kwenye Recovery ( Team Win Recovery Project)

Kama tulivyokwishaona, zoezi la Kuflash linaweza ku fail..na ikitokea Simu Haitawaka Tena!
mpaka Computer na USB vitumike KUFUFUA simu hio Hivyo  kuepuka hili, hua tunahifadhi mfumo uliopo ili likitokea tatizo tuurudishe simu iwake.. Ili kuuhifadhi mfumo uliopo, gusa ‘Backup’ , weka alama kwenye Boot, Unboot, nvram, System,
na Cache,,, gusa Storage na uweke alama kwenye sd card kisha ‘Swipe to Back Up’
Ikishamaliza ku back up rudi nyuma kisha gusa ‘wipe’ ˃ ‘Advanced wipe’ kisha weka alama kwenye Dalvic Cache, System, Cache na Data kisha ‘Swipe to Wipe’ Kumbuka ku format System ndicho kinachofanya Simu isiwake tena kwani OS haipo tena mpaka hatua hii. Kwa hio hakikisha Backing Up Process ilikamilika kabla ya ku format/wipe Simu.

8. Baada ya ku back up na ku wipe, rudi nyuma, gusha ‘Install’, chagua ile ROM ya Simu yako uliokwishai download kisha
‘Swipe to Confirm Flash’. Ni ndani ya Dakika zisizozidi 10, utakua tayari una Android Lollipop experience kwenye simu yako!!!
Gusa Reboot ˃ System

Angalizo
Kuna baadhi ya Lollipop ROMs ambazo System apps hazijawa included. Uwe makini hapo, kama hio ROM haina apps, lazima kuna maelekezo ya ziada ulipoipatia hio ROM.

9. (Hatua hii ni endapo Flashing process ili fail…) Gusa Restore, chagua Package yenye tarehe sahihi kisha Swipe to Restore.
Hapo ule Mfumo uliopo utarudishwa na simu yako ITAWAKA kama kawaida. Kama bado utakua na nia Tafuta ROM nyingine tofauti kisha jaribu tena.

TAHADHARI:
  • Software Support Tanzania, hatutohusika kwa uharibifu wa aina yoyote utakafanywa kutona na Uzembe Au Kutokuwa Makini Kwa Wakati Wa Kufanya Zoezi ili Kwani Kila Kitu kwenye Tovuti hii Kimejribiwa na Kufanya Kazi Ipasavyo.
  • Kwa Msaada Wowote Wasiliana na Watoa huduma wetu wa Software Support Tanzania.
  • Kwa Mahitaji ya ROM sahihi Kwaajiri ya Simu yako Wasiliana na Software Support Tanzania.

Mpaka Hapo Utakuwa Umefanikisha Ku-Update Android Version Ya Simu Yako Kutoka Kwenye Kitikat Kwenda Kwenye Lollipop.

ili Kuwa Wa Kwanza Kupata Masomo Yetu

Download App Yetu Playstore hapa Chini 
Jiunge na WhatsApp group letu hapa

USISAHAU KUSHARE MAKALA HII NA WENZIO.


Imeandaliwa na SOFTWARE SUPPORT TANZANIA

Kwa mawasiliano Zaidi aanasi kupitia

Facebook Page: Software support Tanzania

Instagram: Softwaresupporttanzania

Email: softwarestanzania@gmail.com

BLOG: http://softwaresupporttz.blogspot.com/

Don’t forget to subscribe our BLOG and Youtube channel Software support Tanzania

Usisahau ku-share kwa ndugu, jamaa na marafiki.



NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...