Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Test link

FAHAMU MATUMIZI MATANO YA KAMERA YA SMARTPHONE YAKO




Habari…

Tumaini letu wote mnaendelea vizuri na leo tunafundisha matano tofauti tofauti ya Camera ya simu yako ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kurahisisha maisha.
Kuna matumizi mengi sana ya kamera ya simu janja zetu ukiachana na yale tuliyo yazoea ya kupiga picha tu

YAFUATAYO NI MATUMIZI MATANO MUHIMU YA CAMERA YAKO

1. SCAN NYARAKA

Kamera ya simu janja yako pia inaweza ikawa ina’scan’ nyaraka tofauti tofauti. Pata picha unakuwa na ‘scanner’ ambayo ipo mfukoni kwako. Unaweza uka ‘scan’ vitu kama vile mikataba,risiti au kitu chochote kilichopo katika karatasi na unataka ukifanye kiwe kidigitali

Baada ya hapo unaweza ukaamua kutuma vitu hivyo katika barua pepe au unaweza ukavihifadhi katika mfumo wa PDF au JPG
JINSI YA KUSCAN
Kwa iOS download Evernote
Kwa Android shusha Google Drive ndani yake kuna kipengele cha ku’Scan’

2. TUNIA CAMERA YA SIMU KAMA MKALIMANI WAKO
Teknolojia inabadilisha dunia kwa kiasi kikubwa sana miaka kadhaa iliyopita ningebisha kata kata kama jambo hili lingeweza kutokea. Hivi unajua unaweza ukatumia kamera ya simu yako ili kutafsiri lugha Fulani?
Kumbuka kuna maandishi huwa yanaandikwa na mara nyingi tunakuwa hatuyaelewi kwa mfano ukiwa katika mgahawa ikaja menyu yenye maandishi ya kigeni hapo ndipo huduma hii utakapo ona ubora wake
Ukiwa na App ya Google Translate, ambayo inaweza kutafsiri lugha 29 utafanikisha hilo kwa kuweka kamera mbele ya maandishi yaliyoandikwa na hapo App itafanya zoezi zima la kutafsiri kwenda katika lugha unayotaka

3. TUMIA CAMERA YA SIMU KWA ULINZI

Hivi ulishawahi kuwa na hamu ya kutumia kamera ya simu yako kama njia ya ulinzi? Labda una kamzigo kako pale ndani na unataka ukachunge. Ondoa shaka kuna App maalum ambazo zinakuwezesha kufanya hayo yote. App hizi hutumia kamera ya simu janja ili kugundua mwondoko wa aina yeyote (motion) na kisha kukutaarifu kupitia barua pepe (e-mail) yako
Kwa Android shusha App ya Silent Eye

4. FUATILIA BARCODES ZA UPC
Wakati mwingine wakati ukiwa unafanya manunuzi ya vitu na ukawa huna uhakika kama unanunua vitu imara achana na ku Google, tumia kamera ya simu janja yako kuweza kuichunguza bidhaa hiyo.
Zile App ambazo zinamsaidia mtu ku’scan code’ za UPC zinampatia mtu taarifa za bidhaa katika kiganja chake kabisa. Ukiachana na taarifa kuhusiana na bidhaa bado utaweza kufananisha bei tofauti tofauti ya bidhaa hizo ili kujua kama umepewa bei nzuri au la
Kwa Android shusha App ya ShopSavvy Barcode and QR Scanner

5. SHANGAA ANGA
Hivi ushawahi kukaa usiku na ukawa unashangaa anga na ukaanza kujiuliza maswali kama baadhi ya vitu unavyoviona ni nyota au ni sayari zingine? kama jibu ni ndiyo endelekua nasi.
Download App ya Skyview kwa Android na iOs itakupa majibu yote
App hii inatumia Camera ya simu yako katika kukuonyesha jinsi anga ilivyo cha kufanya hapa wewe elekeza Camera ya simu janja yako katika anga.

Download App Yetu hapa Chini
http://www.mediafire.com/file/66js1vkjolpg68s/Software+Support+Tz.apk

USISAHAU KUSHARE MAKALA HII NA WENZIO.

 Imeandaliwa na SOFTWARE SUPPORT TANZANIA

Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana nasi kupitia
Facebook Page: Softwaresupporttz
Instagram: Softwaresupporttanzania
Email: softwarestanzania@gmail.com
BLOG: http://softwaresupporttz.blogspot.com
YOUTUBE CHANNEL: Software Support Tanzania
Don’t forget to subscribe our BLOG and Youtube channel Software support Tanzania
Usisahau kushare darasa hili na wenzako wa karibu
Thanks…..
NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...