Habari...
Tumaini letu wote mnaen
delea vizuri, Leo tutafundisha ni namna gani
unaweza kuifanya simu yako idumu na chaji kwa muda mrefu
MAHITAJI
Wote tunajua kwa hapa Afrika na Tanzania kwa ujumla simu za Android kama tecno ni moja ya simu zinazotumiwa sana, lakini simu hizi huwa na matatizo mbalimbali na moja kati ya tatizo hilo tutaenda kuliongelea leo ambalo ni kuisha kwa chaji haraka.
Mara nyingi hatua za kudhibiti chaji kupungua kwenye simu za Android ni sawa na zile za kudhibiti kupungua kwa chaji haraka kwenye simu nyingine, lakini njia tutakazo ongelea hapa nyingi zitakuwa zikihusisha simu za tecno. Unaweza pia kujaribu njia hizi kwenye simu yako ya kawaida ya Android.
HATUA
#1. Punguza Sauti ya Muito
Simu nyingi za android zimetengenezwa kwa kutumia spika zenye kutumia mzunguko wa coil , ambazo mara nyingi spika hizi huwa ndogo tofauti na simu nyingine, mara nyingi kutokana na udogo wake na mzunguko wa coil hizi utumia kiasi kikubwa cha chaji ya ziada pale zinapo toa mlio hivyo kufanya chaji ya simu yako kuisha kwa haraka. Ni vyema kuakikisha sauti ya muito wa simu yako iko kwa kiasi cha kawaida kupunguza matumizi ya ziada ya chaji.
#2.Safisha Battery ya Simu yako au Chaji ya Simu Yako
Hapa kuna njia mbili tofauti kwa simu mbili tofauti, Kama simu yako inatoka battery au kama simu yako inafunguka kwa nyuma sehemu ya Battery ni vyema ukachukua muda wako kutoa battery ya simu yako na kusafisha kwenye vikoili vya mbele vya battery yako vinavyo gusana na sakiti ya simu yako. Hii itasaidia kuondoa uchafu (Carbon) unaoweza kuzuia chaji kwenye simu kuingia vizuri ndani ya battery ya simu yako.
#Vilevile kama huenda simu yako haifunguki kwa nyuma sehemu ya kuweka battery, basi unaweza kusafisha kichwa cha waya wa chaja ni hii itasaidia endapo kuna uchafu unaozuia battery yako kuingia chaji vizuri pale unapochaji.
#3. Chaji Simu yako huku umewasha (Flight Mode)
Sehemu ya flight mode ipo kwenye kila simu, sehemu hii itakusaidia kuzima network kwenye simu yako ya pale unapokua unataka kutumia simu yako bila kuwa na mawasiliano ya kimtandao. Sasa ukichaji simu yako uku umewasha sehemu hii inaruhusu simu yako kujaa chaji vizuri kwani chaji inayo ingia haitumiki kwa kasi kubwa na hivyo battery kujaa chaji kwa haraka zaidi na kikamilifu.
#4.Hakikisha Simu yako Inaisha Chaji Ndipo Uchaji Tena
Hakikisha smu yako inaisha chaji ndipo uchaji tena, njia hii ni muhimu sana kwani inasaidia battery yako kuweza kudumu zaidi kwani kuisha kwa chaji yote ndipo kunapo tegemeana sana na kudumu kwa chaji ya battery.
Yaani fikiria hivi, “maji yakikaa sana huaribika na ili kupata maji fresh ni vyema umwage kwanza yale yalio kaa kwa muda mrefu na ndipo uweke maji mengine masafi, kwa mtindo huo maji hayo mapya yatadumu zaidi kuliko kuongezea maji masafi juu ya maji ambayo yalikuwa yamesha kaa kwa muda mrefu” hivyo ndivyo battery ya simu inavyo fanya kazi, hakikisha angalau kila baada ya siku mbili una hakikisha battery ya simu yako inaisha kabisa ndipo uchaji upya.
#Muhimu
Kuchaji Bettry ya simu yako pasipo bettery kuisha chaji kabisa kwakipindi kirefu nolo pia ni tatizo ambalo linapelekea bettery kupoteza ufanisi wake.
#4.Epuka kuchaji Simu yako Kwenye Joto Kali
Kwa wale ambao tunaishi Dar es salaam, najua kuwa joto ni kali ndio maana hapa Dar es salaam simu nyingi zinaharibika battery kuliko hata mikoani, japo kuwa hii inategemeana na ubora wa battery lakini ni kweli kuwa kuchaji battery mahali kwenye joto kali sana husababisha battery ya simu yako kuharibika haraka. Sasa basi ili kudhibiti simu yako kuisha chaji haraka na battery yako kuharibika, hakikisha unachaji simu yako ikiwa haijavikwa kava na ni vizuri kuchaji kwenye soketi ya umeme isiyo na msongamano wa vitu vingi.
#5.Epuka kabisa kuchaji Bettery yako kwenye kobe
Kuchaji bettery ya simu yako kupitia kobe kunachangia kuharibika na kuondoa ufanisi wa bettery yako kwa kiasi kikubwa hii yote kutokana na kobe haina uwezo wa kuzuiya umeme kwendelea kutembea hata kama bettery lako litakuwa limejaa kama ilivyo kwenye simu na hii ndiyo sababu inayopelekea bettery kuvimba na kupoteza ufanisi wake.
#6.Ondoa Wallpaper zinazo tembea au kubadilika badilika kwenye simu
Kubadilika badilika au tembea kwa Wallpaper kwenye simu yako kunachangia bettry yako kupoteza ufanisi wake wa kuifadhi chaji hatakama utakuwa auitumii,hii nisawa na kuwa unacheza game tu kwenye simu yako muda wote isipokuwa Game inatumia vitu vingi kama vibration na Sound hivyo epuka kuweka picha za mtindo huo kwaenye wallpaer yako.
#7.Punguza kiasi cha mwanga_kwenye_simu_yako
Mwanga wa simu pia nao hutumia chaji nyingi ya betri la simu yako, na hususani ikiwa kioo cha simu yako ni kikubwa na mwanga ni mkali. Hivyo ni vizuri kupitia mpangilio wa mwanga wa simu yako na kuupunguza kwa kiasi ili kusaidia utunzaji wa chaji. Pia kumbuka kuzima mwanga wa simu unapokuwa huitumii ili kutunza chaji
#8.Punguza Application amabazo huzitumii kwa muda mrefu
Kama kwenye simu yako kuna Application nyingi basi ni lazima simu yako itakuwa inaisha chaji mara kwa mara. Ili kuhakikisha kuwa battery ya simu yako ya inadumu zaidi hakikisha unaondoa programu zisizo na ulazima na acha zile ambazo una matumizi nazo ya kila siku. Unaweza kuondoa programu ambazo huzitumii kila siku na pale unapo ziitaji unaweza kuzipakua tena kuliko kubaki nazo kwenye simu bila matumizi ya muhimu ya kila siku.
#8. Hakikisha Bluetooth, GPS (Location) na Wi-Fi Zimezimwa
Programu nyingi mbalimbali huwa na uwezo wa kuwasha GPS au Location bila hata wewe kujua, sasa mara nyingi unapo maliza kutumia programu hizi GPS huendelea kuwaka hivyo kutumia kiasi kikubwa sana cha data, pamoja na chaji bila hata wewe kujua. Hii ni moja kati ya zile sababu kwanini unakuta kifurushi chako cha data au (Bando) kimeisha bila hata wewe kutumia.
#9. Tumia “Battery saving Mode”
Kutumia “Battery saving Mode” inafanya simu yako itumie chaji kwa kiwango kidogo sana, kwa sababu unapotumia mfumo huu simu yako hufunga apps zote zisizo muhimu na kuacha zile za muhimu tu zifanye kazi.
#10.Usisikilize mziki kwenye Internet
kusikiliza mziki kwenye internet yani “ku-stream” bila kikomo kwa kutumia application kama vile “Dizzer” Mziki na nyingine nyingi, kila unapotumia application hizi au internet yenyewe kusikiliza mziki chaji yako inapungua kwa haraka zaidi kwani kama nilivyo eleza awali ni lazima simu yako itumie server za application hiyo au website uliyotembele ili uweze kusikiliza mziki, hivyo basi hii usababisha chaji yako kupungua kwa haraka kuliko kawaida.
#hayo ndio mambo ambayo ni ya msingi sana kuyafanya kama unataka simu yako iweze kudumu na chaji, unaweza kuyafanya kwenye simu yoyote ya Android ili kuweza kuongeza ufanisi wa battery yako pamoja na kudumu kwa chaji kwa simu yako.
Download App Yetu hapa Chini
USISAHAU KUSHARE MAKALA HII NA WENZIO.
Imeandaliwa na SOFTWARE SUPPORT TANZANIA
Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana nasi kupitia
Facebook Page: Software support Tanzania
Instagram: Softwaresupporttanzania
Email: softwarestanzania@gmail.com
BLOG: http://softwaresupporttz.blogspot.com/
Don’t forget to subscribe our BLOG and Youtube channel Software support Tanzania

