Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Test link

JINSI YA KUINSTALL WINDOW 7 KWENYE COMPUTER




Habari…
Tumaini letu wote mnaendelea vizuri na leo tunafundisha ni jinsi gani unaweza kuinstall au kupiga window kwenye computer
Zifuatazo ni hatua za kufata ila kufanikisha zoezi hili.

MUHIMU
· Fanya backup ya vitu vyako vyote vilivyopo local disk C kwenye computer yako
· Fuatilia hatua zote kwa umakini.
· Unatakiwa kufahamu BOOT OPTION ya Computer yako kutegemea na aina ya computer yako.
.Usb bootable au window dvd bootable

HATUA ZA JINSI YA KUISTALL WINDOW 7
Hatua ya 1.
Weka Usb flash yako au Window DVD yako kwenye computer husika unayohitaji kupiga window.

Kama unavyoona kwenye picha hapo chini


Hatua ya 2.
Restart au zima kabisa computer yako,kisha bonyeza boot menu button mara nyingi nyingi wakati inaendelea kuwaka,hii utokan ana aina au model ya computer husika.
kama inavyoonekana hapo chini kwenye picha.

Kwa mfano.
Kama model ya computer yako ni Dell utabonyeza F12 wakati inawaka
Kama inaavyoonekana kwenye picha hapo chini

Hatua ya 3.
Baada ya kubonyeza boot menu button mara nyingi nyingi itakuleta kwenye boot menu kisha chagua kifaa ambacho unatumia kupigia window kama ni CD/DVD/CD-RW DRIVE au USB FLASH.
Hapa tunatumia CD hivyo utabonyeza kwenye CD/DVD/CD-RW Drive.
Kama picha inavyoonesha hapo chini.



Hatua ya 4.
Window itaload files zilizokuwepo kwenye CD yako kwaajiri ya kufanya installation.
Kama unavyoona kwenye picha hapo chini


Hatua ya 6.
Baada ya window ku-load mafile utabonyeza kwenye neno INSTALL NOW
Kama unavyoona kwenye picha hapo chini


Hatua ya 7.
Kisha utaweka alama ya tick kwenye neno I ACCEPT THE LICENSE TERM.
Kama unavyoona kwenye picha hapo chini


Hatua ya 8.
Kisha utachagua kwenye neno (CUSTOMER (ADVANCED)
Kama unavyoona kwenye picha hapo chini


Hatua ya 9.
Zitakuja partition zote zilizokuwepo kwenye computer yako hapo awali cha msingi unachotakiwa kujua ni kwamba partition itakayooneka na kivuli ndiyo partition iliyokuwa na window yako ya hapo awali hivyo hakikisha una-format partition hiyo kabla ya kuendele na hatua zingine.
Kama unavyoona kwenye picha hapo chini.


Hatua ya 10.
Baada ya hapo utachagua kwenye partition uliyotoka kui-format kisha utabonyeza kwenye neno NEXT.
Kama picha inavyoonesha hapo chini
 
Hatua ya 11.
CD/DVD/CD-RW itaanza kufanya Window installation process kwenye computer yako hivyo utasubiri imalize asilimia zote (0%-100% completing)
Kama unavyoona kwenye picha hapo chini

Hatua ya 12.
Baada ya hapo computer itaji-restart na kuendelea automatically kisha utapangilia muda na tarehe kwenye computer yako,hapo kwenye muda (time zone) utachagua Nairobi na kubonyeza NEXT.
Kama picha inavyoonekana hapo chini

Hatua ya 13.
Baada ya hapo utajaza details zako kama jina lako,password yako n.k
Kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini
 
Hatua ya 14.
Baada ya hatua ya 13 itakuomba product key za window husika utabonyeza NEXT kuruka hiyo hatua.
Kama unavyoona kwenye picha hapo chini

Hatua ya 15.
Utachagua network unayohitaji kutumia kwenye computer yako kama Home Network, Work NETWORK, PUBLIC NETWORK kulingana na matumizi yako.
Kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini

Hatua ya 16
Mpaka hapo utakuwa umeshamaliza kufanya window installation na kuanza kuitumia computer yako.
Kama picha inavyoonekana hapo chini


MUHIMU
Mpaka hapo utakua umefanikisha hatua zote za kuinstall/kupiga window 7 ila window haitafanya kazi kwa ufanisi unaohitajika kutokana na ukosefu wa product key ili kuweza kupata Software Yetu Yenye Uwezo wa Kufanya Activation Za Window Zote Pamoja na za MS Office utalipia kiasi cha Tsh 5,000/=









NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...