Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Test link

JINSI YA KUANDIKA MESEJI KATIKA MIANDIKO TOFAUTI TOFAUTI KWENYE WHATSAPP




Habari…
Tumaini langu wote ni wazima na mnaendelea vizuri..

Leo tutawaelekeza ni jinsi gani unaweza kuandika fonts/miandiko tofauti tofauti kwenye message za WhatsApp, kwa sababu kuna wakati mwingine unakua unataka kuonyesha Kichwa cha habari ama msisitizo wa neno kwa ku-bold ama ku-highlight kipengele katika sentensi yako au kuonesha utofauti katika ujumbe wako wa message WhatsApp ili kufanya hayo yote unatakiwa kufata hatua zifuatazo.


Kwa leo tutaonesha fonts nne tofauti tofauti.

MUHIMU.

1. Zingatia maelekezo na hatua zote kwa ufasaha.
2. Code hizi zitafanya kazi kwenye Application ya WhatsApp pekee.
3. Alama zitakazo tumika hazita onekana kwa msomaji wa SMS yako.

MAHITAJI

1. Simu yoyote ya Smartphone Android, Window phone, IOS
2. Application ya WhatsApp kwenye simu yako.

HATUA

1. Kufanya herufi ziwe na mistali katikati katika ujumbe utakao tuma..

ili kufanya herufi ziwe na mistali katikati unapomtumia mtu SMS whatsapp.Weka alama hii (~) mwanzo na mwisho wa ujumbe wako bila kuweka alama ya mabano.

Kwa mfano neno mambo liwe hivi ~mambo~

2. Kufanya herufi ziwe zimekolea na rangi nyeusi (bolded).

ili kufanya ujumbe wako uwe umekolezwa na rangi nyeusi utatuma ujumbe wako kwa kuanza na alama hii (*) na kuishia na alama hiyo hiyo.

Kwa mfano. neno Hello software Support Tanzania utaiandika hivi *Hello Software Support Tanzania*

3. Kufanya mwandiko uwe umelala na kupauka.

ili uweze kufanya muandiko wako au ujumbe wako uonekane umelala na kupauka kwa wasomaji wako. utaandika code hii ( _ ) mwanzo na mwisho wa ujumbe wako bila kuweka alama ya mabano.

Kwa mfano. Neno Hello Software Support Tanzania utaandika hivi _Hello Software Support Tanzania_

4. Fufanya mwandiko kwenye ujumbe wako uwe wa kusimama na kupauka.

ili muandiko wako na ujumbe wako uonekane wa kusimama na kupauka unatakiwa uandike code hizi kama zilivyo (```) utaandika zote tatu mwanzo na mwisho wa ujumbe wako

Kwa mfano. Neno Hello Software Support Tanzania utaandika hivi ```Hello Software Support Tanzania```

Mpaka hapo nakifiri tutakuwa tupo pamoja na utawezewa kubadilisha muonekano wa SMS zako wa wasomaji wako wote kadrii utavyopenda kuziweka.

Imeandaliwa na SOFTWARE SUPPORT TANZANIA
Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana nasi kupitia
Facebook Page: Software support Tanzania
Instagram: Software_support_tanzania
Email: softwarestanzania@gmail.com
BLOG: http://softwaresupporttz.blogspot.com/

Usisahau kushare darasa hili na wenzako wa karibu
NextGen Digital Welcome to WhatsApp chat
Howdy! How can we help you today?
Type here...